

Dar es Salaam, Tanzania – Aprili 2025 – Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Musa Hassan Zungu na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Janabi leo wamepokea vifaa vyenye zaidi TSh 2,552,580,000.00. kutoka shirika lisilo la kiserikali la Qatar Charity.
Kwa kushirikiana na walengwa na jamii, Qatar Charity (QC) inalenga kuendeleza uhusiano kati ya shughuli za misaada ya dharura na miradi endelevu ya maendeleo ya kijamii.
Katika utekelezaji wa shughuli zake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kibinadamu na maendeleo, Qatar Charity imejikita kwenye misingi ya ushirikiano kama usawa, uwazi, uwajibikaji na ujumuishaji. Pia, Qatar Charity inazingatia misingi ya kibinadamu kama vile uhuru, kutokufungamana na pande zozote, na usawa.
Kwa zaidi ya miaka thelathini, Qatar Charity imeendelea kukua kwa kasi katika nyanja za utekelezaji wa miradi na uimarishaji wa taasisi. Hivi sasa, Qatar Charity inafanya kazi katika zaidi ya nchi 70 duniani, ikiwa na ofisi za uwakilishi katika nchi 34.
Qatar Charity ni mwanachama wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1997 na ni mshiriki wa mitandao na majukwaa mbalimbali ya kimataifa, likiwemo START Network. Tangu 2009, Qatar Charity pia ni miongoni mwa mashirika yaliyo tia saini.
Kanuni za Maadili za Harakati ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu.
Katika kuendeleza mchango wake kwa Tanzania, shirika hili limetoa msaada wa vifaa muhimu
vya tiba na elimu kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ikiwa ni Pamoja na:
Ø 110 Viti vya Magurudumu
Ø 30 Mashine za kupima shinikizo la damu
Ø 30 Meza za Watoto
Ø 30 Viti vya Watoto
Ø 5 Mitungi ya Kuchuja Maji
Thamani ya msaada huu mahsusi kwa Hospitali ya Muhimbili ni TSh 52,812,000/=.
Sherehe rasmi ya makabidhiano ilihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Mussa Azzan
Zungu, Mbunge wa Jimbo la Ilala na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, ambaye alisifu mchango wa QC na kuonesha jinsi unavyooana na ajenda ya kitaifa
ya maendeleo:
“Mchango huu ni ishara ya mafanikio yanayoweza kupatikana pale ambapo ushirikiano
ukiambatana na uongozi thabiti. Chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu
Hassan, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za afya, elimu, na ustawi
wa jamii. Juhudi za Qatar Charity zinachangia moja kwa moja kutimiza vipaumbele hivi na
kusaidia kufanikisha mipango ya maendelo ya serikali,” alisema Mheshimiwa Zungu.
Pia Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mtaalamu mashuhuri wa afya ya moyo, ambaye alipokea msaada kwa niaba ya hospitali na kueleza:
“Mchango huu utagusa maisha ya mamia ya wagonjwa, hasa wale wanaohitaji vifaa vya kuwasaidia kutembea na huduma za watoto. Ushirikiano kama huu ni muhimu kwa kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini.”
Bw. Amjad Al Tahhan, Mkurugenzi wa Qatar Charity Organization nchini Tanzania, alieleza dhamira ya muda mrefu ya shirika hilo katika sekta ya kibinadamu na maendeleo:
“Lengo letu ni kuinua jamii kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, maji safi, na fursa za kiuchumi. Ushirikiano wetu na taasisi kama Muhimbili ni sehemu ya juhudi pana za kujenga suluhisho endelevu kwa ajili ya mustakabali wa Taifa la Tanzania.”
Kazi za Qatar Charity nchini Tanzania zinaangazia maeneo mbalimbali muhimu kama afya, elimu, WASH (Maji, Usafi wa Mazingira na Usafi Binafsi), usalama wa chakula, na uwezeshaji wa kiuchumi. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, miradi yake imewanufaisha maelfu ya Watanzania kupitia shughuli kama vile mgao wa vikapu vya chakula, ujenzi wa shule, usambazaji wa huduma za afya, na ujenzi wa miundombinu ya maji.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!