
Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Amolo Odinga, umewasili nchini Kenya leo asubuhi kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), ukitokea nchini India ambako alikuwa akipokea matibabu.
Rais wa Kenya William Ruto, pamoja na Rais wa zamani Uhuru Kenyatta, familia ya Raila Odinga, na viongozi wakuu wa serikali, wameongoza mapokezi hayo rasmi uwanjani.
Ujumbe maalum kutoka Kenya ulitumwa jana kwenda India kuchukua mwili wa kiongozi huyo mkongwe wa kisiasa, ambaye amekuwa nguzo muhimu katika historia ya demokrasia nchini humo.
Baada ya mapokezi, mwili huo umepelekwa Lee Funeral Home, jijini Nairobi, kwa maandalizi ya taratibu za mazishi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!