Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Nchimbi: CCM ndio Chama Kilichojidhahirisha Kinaweza Kuhangaika na Matatizo ya Wananchi Wake

  • 7
Scroll Down To Discover

MGOMBEA Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema CCM ndiyo chama pekee kilichojidhihirisha kwa Umma, kinachoweza kuhangaika na matatizo ya wananchi wake.

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2025 wakati akihitimisha mkutano wake wa mwisho wa hadhara wa kampeni , uliofanyika kwenye uwanja wa Kazegunga katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake zinazoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.

Amesema, vipo vyama vingi duniani havishughuliki na matatizo ya wananchi wake bali kwa maslahi yao binafsi na viongozi.

Dkt.Nchimbi amesema, chama hicho ndicho kimeudhihirishia Umma kuwa ndiyo chama kinachoweza kuwaletea miradi ya maendeleo wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, biashara, kilimo na miundombinu ya barabara.

Pia, ameeleza, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufuata misingi ya CCM ameweza kuendeleza na kukisimamia chama na kuhakikisha kinaendelea kuwa na misingi mizuri na chama imara nchini.

Aidha,Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kumuombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Ndugu Peter Selukamba pamoja na Madiwani.



Prev Post Serikali Imeweka Mikakati Dhabiti Ya Kukabiliana Na Majanga Nchini-Majaliwa
Next Post Rais wa Madagascar atoroka kufuatia maandamano ya Gez Z, katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook