Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Trump Asitisha Kwa Muda Ushuru Mpya kwa Washirika wa Kibiashara, Aiacha China Nje

  • 10
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha kwa muda wa siku 90 nyongeza ya ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka kwa takriban washirika 60 wa kibiashara isipokuwa kwa China, ambayo imewekewa ushuru wa juu wa hadi asilimia 125.

Katika tangazo lililokuja saa chache tu baada ya ushuru mpya kuanza kutekelezwa, Trump amesema ameamua kuidhinisha “kupunguzwa kwa ushuru wa asilimia 10%” kwa washirika wengine wa kibiashara huku mazungumzo yakifanyika, lakini amechukua msimamo mkali dhidi ya China kutokana na kile alichokitaja kama “ukosefu wa heshima” kutoka kwa Beijing.

“Itafika wakati China igundue kuwa siku za kuvuna kutoka kwa Marekani na nchi zingine sio endelevu au kukubalika,” amesema Trump.

Tangazo hilo linafuatia hatua ya China kulipiza kisasi kwa kutangaza ushuru wa hadi asilimia 84 kwa bidhaa za Marekani, hali iliyoibua wasiwasi wa kuzorota zaidi kwa uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo makubwa kiuchumi duniani.

Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent alisema kuwa mabadiliko haya ya sera hayajasababishwa na anguko la kiuchumi la dunia, lakini viongozi wa chama cha Democrat wamekosoa hatua hiyo, wakisema kuwa Trump “anayumba na kurudi nyuma.”

“Uamuzi huu unaonesha kiongozi anayekosa msimamo, anayebadili mwelekeo kwa shinikizo la kisiasa na kiuchumi,” alisema Chuck Schumer, mmoja wa viongozi wa juu wa chama cha Democrat.

Licha ya mvutano huo, Rais Trump ameonesha matumaini kuwa makubaliano kati ya Marekani na China yanaweza kufikiwa.

“Nadhani Rais Xi ni mtu anayejua anachokifanya. Ni mwerevu, anaiipenda nchi yake, na naamini tutapokea simu kutoka kwake hivi karibuni ili tufikie makubaliano ambayo yatakuwa mazuri kwa wote,” amesema Trump.

Trump amefafanua kuwa hatua yake mpya haiondoi ushuru uliotangazwa awali na unaoendelea kutekelezwa tangu Aprili 2. Hii ni pamoja na ushuru wa asilimia 25 kwa magari na vipuri vya magari kutoka nje na ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zote za chuma na alumini zinazoingia nchini.



Prev Post KISA CAF ….FADLU ARUDISHWA KWAO AFRIKA KUSINI KILAZIMA…ISHU NZIMA IKO HIVI…
Next Post CCM yatangaza mchakato wa uteuzi wagombea wa Ubunge, Ujumbe Baraza la Wawakilishi udiwani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook