
Dodoma, Oktoba 10, 2025 — Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, inatarajiwa leo saa nane mchana kusoma hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Chama cha ACT Wazalendo kupitia Bodi ya Wadhamini pamoja na Luhaga Mpina, kupinga uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi (THEC) wa kuwaengua katika kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kesi hiyo, ambayo imevuta hisia za wadau wa siasa na wanasheria nchini, ilihusu hoja za kisheria kuhusu uhalali wa uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi kuwazuia wagombea wa chama hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.
ACT Wazalendo kupitia mawakili wake walidai kuwa hatua ya Tume ni kinyume cha Katiba na sheria za uchaguzi, huku wakisisitiza kuwa chama hicho kilifuata taratibu zote za kisheria katika mchakato wa uteuzi wa mgombea wake wa urais.
Hukumu hiyo inatarajiwa kuwa ya kihistoria na inaweza kuweka mwelekeo mpya katika tafsiri ya sheria za uchaguzi na mamlaka ya Tume Huru ya Uchaguzi nchini.
Waandishi wa habari na wadau wa demokrasia wamekaribishwa kuhudhuria kusomwa kwa hukumu hiyo moja kwa moja katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma.
Imetolewa na:
Abdallah Khamis
Afisa Habari, ACT Wazalendo
Tarehe: 10 Oktoba 2025
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!