Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Wafunguka Sababu za Kumkamata Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu

  • 12
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amethibitisha kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, kulikotokea jana, Aprili 9, 2025.

Kwa mujibu wa Kamanda Chilya, Lissu amekamatwa kutokana na tuhuma za kufanya uchochezi wa kutaka kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mtuhumiwa huyo (Lissu) anaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kuhusiana na tuhuma hizo.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa vyama vyote vya siasa kuepuka kutoa maneno ya uchochezi, lugha ya kukashifu polisi au serikali, au kuonesha viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.



Prev Post Oparesheni ya TAWA Yaua Fisi 43 Itilima, Bariadi na Maswa
Next Post Pacome Zouzoua Ang’ara Ligi Kuu Bara, Aweka Rekodi ya Tuzo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook