

STAA wa Yanga raia wa Ivory Coast, Pacome Zouzoua ameweka rekodi yake ya kwanza ya kutwaa Tuzo sita za Mchezaji Bora wa mwezi huku akifunga mabao nane akipiga asisti tisa hadi hivi sasa katika Ligi Kuu Bara.
Pacome mwenye uwezo wa kuchezea mpira huku akipiga chenga za mahudhi, amekuwa katika kiwango bora msimu huu baada ya kuhusika katika upatikanaji wa mabao 17.
Muivory Coast huyo hadi hivi sasa inaelezwa ana ofa kadhaa kutoka Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika na bado hajaongeza mkataba mpya Yanga.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!