Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Filamu Ya ‘John Wick 5’ Ipo Kwenye Maandalizi, Keanu Reeves Kurudi Tena!.

  • 13
Scroll Down To Discover

Imethibitishwa kuwa Muendelezo Wa Filamu Za John Wick, ‘JOHN WICK 5’ Sasa Ni rasmi Ipo Kwenye utayarishaji. Keanu Reeves atarudi katika nafasi yake kama John Wick, Chad Stahelski Ataendelea kuwa mwongozaji (Director), Huku Basil Iwanyk pamoja na Erica Lee wakiwa kama watayarishaji (Producers).

Swali la wengi lilikuwa kama Keanu Alishamalizana na filamu hii, kwani John Wick: Chapter 4 ilionekana kama hitimisho kwa Uhusika wake, hasa baada ya filamu kumalizika Kwa Utata Juu Ya Kifo Chake.

Machi 2023 Muongozaji wa Filamu ya ‘John Wick : Chapter 4, Chad Stahelski Alisema mhusika mkuu wa filamu hii Ambaye Ni Keanu Reeves huwenda akapumzika kwenye uandaaji wa Chapter 5 kwa muda mpaka watakapoona mapokezi ya Chapter 4, Hivyo Baada Ya Kupata Mapokezi Makubwa Na Mashabiki Kudai Muendelezo Sasa Imethibitishwa John Wick (Kean Reeves) Atarudi Tena Kwenye John Wick 5 Ambayo Inafanyiwa Maandalizi Kwa Sasa.

The post Filamu Ya ‘John Wick 5’ Ipo Kwenye Maandalizi, Keanu Reeves Kurudi Tena!. appeared first on Wasafi Media.



Prev Post Filamu Ya ‘Spider-Man: Brand New Day’ Kutoka Julai 31, 2026.
Next Post Rapa Sexyyred Adai Ndio Rapa Wa Kike Anayechukiwa Zaidi.
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook