MAGAZETI ya Leo Jumanne 08 April 2025
Rais wa heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema kuwa wakati huu Simba inahitaji umoja na ushiriano kutoka kwa kila Mwanasimba ili kuhakikisha wanashinda mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry
Jumatano hii ya April 09, Simba itakuwa mwenyeji wa Al Masry katika ambao Simba inahitaji kushinda angalau mabao Matatu ili Kufuzu Nusu Fainali.
Mo amesema kuwa hii ni mechi muhimu na kihistoria kwa Simba hivyo ni muhimu mashabiki kujitokeza kwa wingi kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa
“Hii Tunavuka. Kwa neema na mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Huu ni mchezo wa kihistoria. Na kila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa sehemu ya ukurasa huu wa Simba”
“Tunachohitaji sasa ni UMOJA. Mashabiki wote wa Simba, tunawaomba mjitokeze kwa nguvu zote. Tujaze uwanja. Ili mioyo ya wachezaji wetu ipate nguvu na ujasiri wa kupigana hadi mwisho”
“Kwa pamoja tutapambana na Inshallah, Tutavuka,” aliandika Mo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Baada ya kucheza robo fainali ya michuano ya CAF kwa misimu mitano mfululizo, wakati huu Wanasimba wanasema imetosha na wanaitaka nusu fainali
HII TUNAVUKA…!
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!