

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Aidan Anacreth, amesema Global Venture imeendelea kutoa fursa za ajira katika sekta mbalimbali zikiwemo usafiri (hasa madereva wa teksi), huduma za hoteli, na uendeshaji wa viwanja vya ndege. Amesema ushirikiano wa karibu kati ya kampuni hiyo na Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA) umewezesha vijana kupata kazi zenye masharti ya haki na mazingira rafiki ya kazi.

Akielezea utaratibu wa kuomba nafasi hizo, Aidan amesema mchakato huanzia kwa mwombaji kujisajili katika ofisi za Global Venture, kisha hufanyiwa usaili ambapo mara kadhaa waajiri kutoka nje ya nchi huja nchini kufanya mahojiano ya ana kwa ana. Aliongeza kuwa baadhi ya nafasi huhitaji sifa maalum za kielimu au kitaaluma, kutegemea na aina ya kazi husika.
Mbali na huduma za ajira, Global Venture pia hutoa msaada kwa wateja katika mchakato wa kupata pasipoti, visa za kusafiri, na pia hupanga safari za utalii kwenda maeneo mbalimbali ndani ya nchi kama vile Pugu Kazimzumbwi, Bagamoyo na Zanzibar.
Mmoja wa wanufaika wa mpango huo, Mohamed Hassan, ambaye ni miongoni mwa wanaoelekea Dubai, amesema kampuni hiyo imekuwa na mchakato rahisi na wa wazi wa kupata ajira nje ya nchi. Amehimiza vijana wengine kuchangamkia fursa hizo, akisisitiza umuhimu wa kuwa na bidii, moyo wa kujituma, na utayari wa kujifunza katika mazingira mapya.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!