Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amempokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Wizara za jijini Dar es Salaam, Septemba 29, 2025.
Akiwa Wizarani hapo, Mhe. Szijjártó amekutana kwa mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Mhe. Balozi Kombo yaliyofuatiwa na mazungumzo ya pande mbili ambayo yaliwashirikisha wajumbe mbalimbali kutoka Tanzania na Hungary wakiwemo Mawaziri.
Mhe. Szijjártó yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia baina ya Tanzania na Hungary.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!