MAGAZETI ya Leo Jumatatu 07 April 2025
Klabu ya Al Masry imeomba sapoti ya Yanga kuelekea mchezo wake wa mkondo wa pili wa robo fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Simba.
Timu hizo zitakutana Jumatano hii ya Aprili 09,2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Kuanzia saa 10:00 Jioni.
Al Masry imetumia ukurasa wake wa Instagram kuitaja Yanga ikiandika: Tunayo furaha kukutana tena na mashabiki wa Young Africans.
Ikumbukwe kuwa, Al Masry ilishinda mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumatano ya Aprili 02,2025 nchini Misri.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!