
Dua maalum ya kumbukumbu ya siku 40 tangu kufariki dunia kwa Alhaj Omary Rashid Mchengerwa imefanyika leo katika kijiji cha Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.
Alhaj Omary Mchengerwa ni baba mzazi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa, na alifariki dunia tarehe 24 Februari 2025 katika mji mtukufu wa Medina, Saudi Arabia.
Shughuli hii imewaleta pamoja ndugu, jamaa, marafiki, majirani, na viongozi mbalimbali waliokusanyika nyumbani kwa familia ya marehemu kwa ajili ya kumuombea dua.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya kiroho ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar bin Zuberi, ambaye amewaongoza waumini katika dua na mawaidha yenye mafunzo ya maisha na subira.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amin.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!