Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwanaridha Simbu Atoboa Siri ya Ushindi Riadha Tokyo, Aelekeza Shukrani NBC Dodoma Mathon

  • 4
Scroll Down To Discover

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald  Sabi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya kumpongeza Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu (kushoto).Hafla hiyo  ilifanyika jijini Dar es Salaam jana jioni. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John  Akhwari.

Mwanaridha wa kimataifa wa Tanzania na mshindi wa mbio ndefu za Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Tokyo Alphonce Simbu amesema siri kubwa ya ushindi wake kwenye mbio hizo zilizofanyika hivi karibuni nchini Japan ni maandalizi mazuri kupitia mazoezi ya muda mrefu huku akitaja ushiriki na ushindi wake kwenye mbio za NBC Dodoma marathon mwezi Julai mwaka huu kama moja ya kichocheo muhimu kuelekea mafanikio aliyoyapata jijini Tokyo.

Akizungumza jana jioni kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kwa ajili ya kuwasilisha pongezi maalum kwa mwanariadha huyo, Simbu alisema licha ya ushindani mkubwa aliupata kutoka kwa wanariadha wa kimataifa kwenye mashindano hayo ya Tokyo bado aliweza kuhimili ushindani kutokana na maandalizi pamoja na morali kubwa aliyokuwa nayo kufutia ushindi wa awali aliokuwa ameupata kwenye mbio za km 21 za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika mwishoni mwa mwezi Julai jijini Dodoma.

Hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam ilihusisha maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Theobald Sabi, pamoja na wadau wa mchezo wa riadha wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bw Rogath John Akhwari alieambatana na baadhi ya wanaridha akiwemo Simbu.
“Ushiriki na ushindi wangu kwenye mbio za KM 21 za NBC Dodoma Marathon mwezi Julai ilikuwa kama chanzo cha morali niliyokuwa nayo niliposhiriki kwenye mashindano ya kimataifa ya Riadha ya Tokyo. Nilitumia mbio za NBC Dodoma Marathon kama kipimo cha kujua utimamu wangu kimwili na ushindi wangu pale Dodoma ndio ulikuwa mwanzo wa ushindi wangu jijini Tokyo.’’
“Nawashukuru sana waandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya NBC kwa kuandaa mbio zenye ushindani ambazo kwasasa tunazitumia kama kipimo sahihi cha utimamu wetu kabla ya kushiriki mashindani makubwa zaidi ya kudunia,’’ alisema Simbu.

Zaidi Simbu aliwashukuru wadau mbalimbali nchini ikiwemo Serikali na benki hiyo kwa kwa pongezi nyingi kufuatia ushindi wake huku akiwapongeza wadau hao kwa jitahada zao katika kukuza mchezo wa riadha hapa nchini.

“Nimepokea salamu za pongezi nyingi ikiwemo kutoka kwa viongozi waandamizi kabisa wa serikali akiwemo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, nashukuru sana kwa hilo na leo hii nipo hapa kupokea pongezi rasmi kutoka benki ya NBC ambao kiukweli wamekuwa ni wadau muhimu sana kwenye sekta ya michezo ukiwemo mchezo wa riadha. Hatua ya NBC kuandaa tukio hili la pongezi kwangu ni uthibitisho tosha za utambuzi wao kwa mchezo huu riadha…nawashukuru sana’’ alisema Simbu.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Sabi alielekeza pongezi hizo kwa RT pamoja na wadau wengine wa mchezo huo ikiwemo serikali kufuatia mafanikio makubwa yanayoendelea kushuhudiwa kwenye mchezo wa riadha hususani hivi karibuni.
“Kwa niaba ya Bodi na Menejimenti ya Benki ya NBC , natoa shukrani za dhati na maalum kwa uongozi wa riadha Tanzania pamoja na Alphonce Simbu kwa kutuwakilisha vyema katika riadha za kimataifa na kupeperusha bendera ya Tanzania duniani kwa ushindi. Akiwa kama mwanafamilia kinara wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Simbu alitumia muda wa 2:09:48 kwenye mbio hizo za Tokyo na hivyo kuandika sehemu ya historia ya taifa letu…pongezi nyingi sana kwake,’’ alisema Sabi.
Kwa upande wake Rais wa RT, Akhwari aliwasilisha shukrani za wadau mbalimbali wa mchezo huo kwa benki ya NBC kufutia mchango wake mkubwa kwenye mchezo huo huku akiitaja mbio ya NBC Dodoma Marathon kama kipimo sahihi kinachotumiwa na wanaridha wa Kitanzania kwasasa kabla ya kushiriki kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.


“Medali hii aliyoileta Simbu haijawahi kuletwa nchini hapo kabla. Ila imekuja kipindi hiki ambacho NBC Dodoma Marathon imekuwa mbio yenye hadhi zaidi ya kimataifa. Hatua hii ni uthibitisho tosha kuwa kwasasa hapa nchini tuna mbio ambazo tunaweza kuzitumia kama kipimo sahihi kujipima kimataifa na zikatupa majibu sahihi. Hapa tunapozungumza kuna washindi wengine walioshika nafasi ya pili kwenye mbio hizi hizi mwezi Julai nao leo (Jumatano) wamefanya vizuri sana kwenye mbio nyingine huko Afrika Kusini’’ alisema Akhwari.

Alisema kwasasa shirikisho hilo lipo kwenye mchakato wa kutekeleza program ya kisasa ya kuandaa vijana na watoto kwenye mchezo huo ili kuandaa kizazi kijacho kitakachoendeleza mafanikio yanayoendelea kushuhudiwa kupitia mchezo huo.

 



Prev Post Mgogoro Wa Nyumba Msasani: Mjane Aomba Zuio La Muda
Next Post Wasira Aungana na Dkt. Nchimbi Katika Mazishi ya Abbas Mwinyi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook