Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: RC Chalamila Aingilia Mgogoro wa Nyumba Mikocheni Bakharesa

  • 3
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameagiza Alice Haule, mjane wa marehemu Justice Rugaibula, pamoja na mfanyabiashara Mohamed Yusufali, wafike ofisini kwake Ijumaa hii ili kufanya mazungumzo ya pamoja yanayolenga kutosha mgogoro wa ardhi uliosababisha uvamizi wa nyumba ya Alice Tembo Street, Mikocheni Bakharesa.

Tukio la jana lilihusisha maibaunsa kusukuma geti na kuingia ndani ya nyumba iliyopangishwa kwa raia wa Kichina, kisha kuanza kuwashambulia watu waliokuwa ndani. Waingiliaji hao walidai kuwa nyumba imeuzwa Mohamed, na kuwataka wapangaji wa Alice waondoke.

RC Chalamila alifika nyumbani hapo leo Septemba 14, 2025, akamsikiliza Alice pamoja na mwanasheria wa Mohamed, na kuagiza nyumba hiyo isitumike kwa pande zote mbili hadi mgogoro utakapomalizika, ili kuepusha misuguano zaidi.

Taarifa kutoka pande zote mbili zinaonyesha kwamba mume wa Alice alikabidhi hati ya nyumba kwa Mohamed mwaka 2011 bila idhini ya mke wake, jambo ambalo Alice amepinga kwa madai ya alama ya dola gumba iliyotumika kwenye nyaraka kuwa feki. Mohamed anadai nyumba ni yake, huku Alice akiendelea kupinga madai hayo.



Prev Post VODACOM TANZANIA PLC PAMOJA NA CHAMA CHA GOFU TANZANIA WAUNGANA ILI KUUNGA MKONO MCHEZO WA GOFU NCHINI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook