
Hajra Mungula, mwakilishi wa mfanyabiashara aliyeingia kwenye mgogoro na Alice Haule, mke wa Justice Rugaibula kuhusu nyumba iliyopo Mikocheni, iliyosababisha taharuki hapo jana, amefunguka kuhusu kinachoendelea upande wa pili.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mungula amesema nyumba hiyo iliuzwa na marehemu Rugaibula mwaka 2011 na kwamba nyaraka zilizopo, zinaonesha kuwa mkewe (Alice) aliridhia na kuweka alama ya dole gumba kwenye nyaraka.
Chalamila na timu yake wamefika Mikocheni jijini Dar es Salaam, kufuatia taharuki iliyozuka hapo jana, Septemba 24, 2025 ikimhusu mjane Alice Haule aliyevamiwa na kutaka kutolewa kimabavu kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe, Justice Rugaibula.
Chalamila ametoa nafasi kwa pande zote mbili zinazovutana, kuelezea kilichotokea ambapo mengi mapya yanaendelea kuibuka.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!