MAGAZETI ya Leo Jumamosi 29 Machi 2025
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limethibitisha taarifa ya kufunguliwa kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, na sasa ni rasmi mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba dhidi ya Al Masry ya Misri utapigwa uwanjani hapo wiki ijayo.
TFF imepokea taarifa ya kufunguliwa kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF), baada ya ukaguzi uliofanywa na wakaguzi wa shirikisho hilo.
Hata hivyo taarifa ya TFF imesisitiza kuwa CAF inaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea kwenye uwanja huo.
Katika hatua nyingine, baadhi ya mashabiki wa soka wa Tanzania wanaoishi nchini Misri, wamejitokea kuipokea timu ya Simba iliyowasili nchini humo kwaajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo Fainali kombe la shirikisho barani Afrika, utakaochezwa Aprili 02, 2025.
Simba itacheza dhidi ya Al Masry katika Uwanja wa New Suez Kuanzia saa 1:00 Usiku.
Mashabiki hao walijitokeza Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cairo, walikuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania, huku wakonekana kuwa na furaha ya kuipokea timu hiyo kutoka Msimbazi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!