Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 03 April 2025

  • 7
Scroll Down To Discover

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 03 April 2025

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ametangaza kuwa zoezi la kubadilisha tahasusi (combination) kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na vyuo limeanza rasmi Machi 31, mwaka 2025 hadi Aprili, 30, mwaka 2025.

Mbali na hilo, amesema kuwa baada ya matokeo ya kujiunga na kidato cha tano na vyuo kutangazwa, ofisi haitashughulikia changamoto hizo kwa kuwa fursa ya kufanya mabadiliko hayo imeshatolewa.

Kwa mwaka wa kwanza Serikali inakwenda kufundisha tahasusi mpya zilizoanzishwa mara baada ya kufanyika marekebisho kwa mtalaa, uliokwenda sambamba kuboresha Serikali ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.

Sera hiyo ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 ilizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Februari Mosi mwaka 2025, ambayo inalenga katika kuyapa kipaumbele mafunzo ya amali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu, Aprili 2, 2025, Mchengerwa amesema kuwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2024 wanayo fursa ya kubadilisha machaguo ya tahasusi za kidato cha tano na vyuo vya kati na elimu ya ufundi kwenye mfumo wa kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na vyuo.

KUBADILISHA MACHAGUO BONYEZA HAPA



Prev Post MAGAZETI ya Leo Ijumaa 04 April 2025
Next Post MAGAZETI ya Leo Jumatano 02 April 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook