
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imeleta mabadiliko makubwa katika Jimbo la Buchosa kwenye sekta mbalimbali kwa kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Shigongo amesema ni vigumu kumaliza changamoto zote kwa mara moja lakini tunapokwenda ni pazuri zaidi kuliko tulipotoka.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa kata, ambapo pia aliwasomea utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Amesema kuwa maendeleo yanayoonekana kwa sasa Buchosa ni tumaini jipya kutoka kwa Rais Samia hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono.
View this post on Instagram
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!