Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Chadema Kuzuia Uchaguzi ni Kufanya Jinai, G-55 Wanazungumza – Video

  • 9
Scroll Down To Discover

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mrema

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mrema amesema iwapo chama hicho kitatekeleza mpango wake wa kuzuia uchaguzi bila kushirikia itakuwa ni sawa na kufanya jinai.

Mrema amesema hayo leo April 06, 2025 akizungumza na wanahabari juu ya waraka ulioandikwa na kundi la G-55 ambalo ni wagombea ubunge 2020 na watiania wa ubunge wa chama hicho kwa mwaka 2025 ulioandikwa kwenda kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika.

“Kwenye no election njia ambayo chama imetumia tunaona sio sahihi…tunaona hatuwezi kuzuia uchaguzi kwa kuwa nje ya uchaguzi, kujaribu kuzuia uchaguzi huku ukiwa nje itakuwa ni sawa na kufanya jinai”

Mrema amefafanua njia pekee inayoaminiwa na kundi hilo ya kuzuia uchaguzi ni kushiriki kwenye uchaguzi ili wawatumie wagombea kushawishi wananchi kuzuia uchaguzi katika vituo vya uchaguzi.



Prev Post Polisi Unguja Yatoa Onyo Watakaofanya Vitendo Vya Uvunjifu Sikukuu Ya Eid El Fitri
Next Post Uhifadhi Ni Uti Wa Mgongo Wa Sekta Ya Utalii Nchini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook