Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Festo Sanga Aibuka Kidedea Kura za Maoni Ubunge Jimbo la Makete

  • 36
Scroll Down To Discover

Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Makete, Festo Richard Sanga, ameongoza katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwania tena nafasi ya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Katika matokeo yaliyotangazwa rasmi, Sanga alipata kura 4,104, akimshinda kwa tofauti kubwa Dr. Toba Nguvila aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,359. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mfanyabiashara Award Mpandilla aliyepata kura 946.

Wagombea wengine waliokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni:

Prof. Norman Sigalla, aliyepata kura 103

Selina Msigwa, aliyepata kura 21

Kwa ushindi huo, Festo Sanga ameonesha kuwa bado ana uungwaji mkono mkubwa ndani ya chama katika jimbo hilo, na sasa anasubiri uteuzi wa mwisho kutoka kwa mamlaka za juu za CCM ili kujua hatma yake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Festo Sanga (@festosangatz)



Prev Post Makonda Aibuka Mshindi wa Kura za Maoni CCM Jimbo la Arusha Mjini
Next Post Mahakama Yatoa Ulinzi Maalum kwa Mashahidi Kesi ya Lissu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook