Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makamu wa Rais Aungana na Wakatoliki Kuuadhimisha Jubilei ya Parokia Dodoma

  • 41
Scroll Down To Discover

Dodoma – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, ameungana na maelfu ya waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki katika Misa Takatifu ya Upadirisho na ufunguzi rasmi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Kiwanja cha Ndege, iliyopo jijini Dodoma.

Ibada hiyo takatifu imefanyika Julai 5, 2025 katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege, na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya.

Katika mahubiri yake, Askofu Kinyaiya amewahimiza waumini kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa amani, busara na uzalendo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, akisisitiza kuwa uamuzi wa kuchagua viongozi una athari kubwa kwa maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Pia Askofu huyo amegusia matumizi ya teknolojia ya akili mnemba (Artificial Intelligence – AI) na kutoa rai kwa jamii kutumia uvumbuzi huo kwa manufaa ya kijamii na kimaadili, badala ya kuiingiza jamii kwenye maovu, udanganyifu au uharibifu wa maadili.

Katika tukio hilo adhimu, jumla ya Mashemasi watatu wamepandishwa rasmi katika daraja la upadre. Waliopewa daraja hilo ni:

Padre Joseph Ibrahim

Padre Sajilo Mark

Padre Damian Mtanduzi

Aidha, Misa hiyo pia ilihusisha tukio maalum la uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo la Katekesi, ambalo litakuwa maalum kwa kufundishia masomo ya dini kwa watoto na waumini wa Parokia hiyo.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango alipongeza Parokia ya Kiwanja cha Ndege kwa kuadhimisha miaka 50 ya huduma ya kiroho na kijamii, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini katika kulijenga taifa lenye misingi ya amani, maadili na maendeleo.



Prev Post RC Siro Asisitiza Umuhimu wa Ushirikiano Kati ya Serikali na Dini
Next Post Yanga Yaanza Mazungumzo na Dickson Job Kuhusu Mkataba Mpya
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook