
Alice Hause ambaye ni Mjane wa marehemu Justice Rugaibula leo September 25,2025 amewasilisha maombi madogo Na.24541/2025 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, akiomba zuio la muda la kutoondolewa kwenye nyumba iliyopo Kiwanja Na.819, Hati Na.49298, Msasani Beach, Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania, Gerard Julius Chami, imesema kwa mujibu wa taarifa ya Msajili Mkuu wa Mahakama shauri hilo na shauri jingine la pili alilofungua Alice yote mawili yako katika hatua mbalimbali Mahakamani.
Taarifa ya Chami imesema “Mnamo tarehe 23 Septemba, 2025, Vyombo mbalimbali vya Habari vilitoa taarifa kuhusu shauri la Madai ya Ardhi lililoko katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Dar es Salaam, linalohusu umiliki wa nyumba iliyopo Kiwanja Na.819, Hati Na.49298, eneo la Msasani Beach, Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam”
“Tarehe hiyohiyo, 19 Septemba, 2025; Wakili wa Bi.Alice, Bw.Mwesiga Muhingo aliwasilisha upya maombi ya kufungua shauri la Madai ya Ardhi katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, hata hivyo, Hati ya Madai aliyowasilisha ilikuwa na mapungufu ya Kisheria, hivyo maombi yake hayakusajiliwa na aliagizwa kufanya marekebisho, aidha baada ya kurekebisha Hati ya Madai, mnamo tarehe 24 Septemba, 2025; shauri lake lilisajiliwa na kupewa Na.24396/2025, likiwa na marekebisho aliyoyaomba ya kumuongeza Msajili wa Hati kama Mdaiwa”
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!