Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mradi wa Liganga na Mchuchuma Utaboresha Sekta ya Viwanda Tanzania

  • 15
Scroll Down To Discover

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema mradi wa makaa ya mawe wa Liganga na Mchuchuma ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele ya kitaifa inayotarajiwa kuchochea utekelezaji wa ajenda ya ujenzi wa viwanda na kuiweka Tanzania katika nafasi ya nne barani Afrika kwa uzalishaji wa madini ya chuma.

Akizungumza leo Septemba 24, 2025 jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini, Prof. Mkumbo amesema hatua zilizopigwa hadi sasa zinaonesha maendeleo mazuri na zinaendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Mradi huu wa makaa ya mawe wa Liganga na Mchuchuma ni muhimu katika utekelezaji wa ajenda ya kitaifa ya ujenzi wa viwanda kama moja ya sekta za kimageuzi. Katika Dira tumeainisha sekta tisa za kimageuzi, na moja wapo ni viwanda vya uchakataji. Hivyo mradi huu unatarajiwa kuwa na nafasi kubwa katika kufanikisha dira hiyo,” amesema Prof. Mkumbo.

Amebainisha kuwa serikali imelenga kuhakikisha chuma kinachozalishwa kinachakatwa na kuongezewa thamani ndani ya nchi ili kutoa nafasi zaidi za ajira kwa vijana wa Kitanzania kupitia mnyororo wa uzalishaji.

Vilevile, Prof. Mkumbo amesisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya taifa, akieleza kuwa mazingira bora ya uwekezaji na biashara ndiyo msingi wa kukuza sekta hiyo. Alisema tayari serikali imeunda timu ya kupitia upya mipango ya kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kurahisisha shughuli za wafanyabiashara, wajasiriamali wadogo na wa kati.

“Lengo letu ni kuhakikisha sekta binafsi inakuwa huru na wazi ili iweze kuzalisha faida, mtaji na utajiri, na hatimaye kufanikisha ndoto ya taifa la kufikia uchumi wenye thamani ya dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050,” ameongeza Prof. Mkumbo.

RC CHALAMILA ALIVYOSHTUKIZA NYUMBANI kwa MJANE ALICE ALIYEVAMIWA na KUTOLEWA NJE KIMABAVU..



Prev Post Polisi Waanza Uchunguzi wa Video ya Askari Kulala Chini – Video
Next Post Jenerali Mkunda Ampongeza Sajinitaji Simbu 
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook