
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ameeleza kuwa amekubaliana na matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 16, 2025, ambayo yameonyesha kwa sehemu kubwa kushindwa kwake na kumpa ushindi mpinzani wake, Prof. Arthur Peter Mutharika.
Kupitia barua yake iliyotolewa Septemba 24, 2025, Rais Chakwera amesema kuwa baada ya kukubaliana na matokeo hayo, aliamua kumpigia simu mpinzani wake kumpongeza na kumtakia heri katika uongozi wake unaokuja.
“Nimefanya hivi kwa sababu nimekubaliana na matokeo ya uchaguzi yaliyothibitishwa na kutangazwa na tume yetu ya uchaguzi, kama ambavyo nitakubali matokeo ya jumla ya mwisho yatakayotangazwa na tume,” imeeleza barua ya Rais Chakwera.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!