
Arusha, Tanzania,Wananchi wa Mkoa wa wamepewa elimu kuhusu Matumizi ya Nishati safi ya Kupikia Katika maonesho ya moja kwa moja Katika mitaa ya Mkoa huo.Wamanchi hao wamepewa elimu hiyo ambapo Wananchi wamejifunza kupitia maonesho ya moja kwa moja juu ya matumizi ya umeme kupikia, kampeni hiyo inayoendeshwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Ukaid na MECS ikiwa na lengo kufikia 80% ya kaya kutumia nishati safi ifikapo 2034.
Aidha mapinduzi hayo Watanzania namna ambavyo wanapika yanaendelea kushika kasi, safari hii yaliingia Arusha na Wananchi walijitokeza kushiriki kwenye maonesho ya moja kwa moja yaliyoonesha faida na urahisi wa kutumia umeme kama nishati safi ya kupikia na wameyapokea kwa ukubwa.
Kampeni zinatarajiwa kuendelea katika mikoa mengine mbalimbali nchini kuhakikisha kila mtu anapata elimu ya kutosha kuhusu usalama wa nishati safi ya kupikia ya umeme.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!