Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NYUMA YA PAZIA HUU…HIZI HAPA SABABU ZA FEI KUBAKI AZAM….SIMBA WAMKANA KWEUPEEE…

  • 2
Scroll Down To Discover

JUMANNE ya Agosti 12, 2025, nyota wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ alisaini mkataba wa nyongeza wa mwaka mmoja utakaomfanya asalie Chamazi hadi 2027. Ilikuwa ghafla sana kwa uongozi wa Azam kwani hawakutegemea jambo hilo kutolea muda huo.

Fei Toto alipewa mkataba mpya tangu Oktoba, mwaka jana, wakati akiwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ katika maandalizi kuekelea Kinshasa, DRC kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya wenyeji. Akaupokea na kuahidi atasaini, lakini hakusaini. Akawa anawapiga danadana kila walipojaribu kumkumbusha. Zikaanza kuibuka tetesi za kutakiwa na Simba na Yanga.

Wachambuzi kadhaa wakauaminisha umma kwamba Fei Toto huenda atavuka wilaya kutoka Temeke hadi Ilala – mitaa ya Kariakoo.

Kwa matajiri wa Azam FC wakadhani tatizo ni dau – likaongezwa, lakini bado Fei Toto aliendelea kuwazungusha huku kelele kwamba vigogo wa Karikaoo wameshamalizana naye na kilichobaki ni kutinga Azam kuwalipa dau wanalotaka ili akazitumikie timu hizo.

Ila niligusia hasa vilongwa mbali na vitendwa mbali. Basi buana, hali ilienda hivyo kwa Fei Toto kudengua hadi uongozi ukakata tamaa na kuacha muda uongee. Hali iendelea kuwa hivyo hadi safari hii aliposaini. Na ni yeye mwenyewe ndiye alipiga simu kwa viongozi na kuwaambia kwamba sasa yupo tayari kusaini.

KWANINI?

Siku zote Fei Toto hakutaka kuongeza mkataba wake Azam akitaka kujiridhisha na dhamira ya klabu hiyo kupata mafanikio.

Fei Toto anataka mafanikio ya uwanjani, sio tu ya kwenye akaunti za benki, na hakuridhika na mambo yalivyokwenda msimu uliopita.

Timu iliyojengwa kumzunguka mchezaji huyo haikuwa na watu alioamini watamsaidia kupata mafanikio. Msimu wake wa kwanza 2023/24 ulikuwa bora akizungukwa na watu kama Kipre Jr na Prince Dube ambao uliofuata (2024/25) hawakuwa sehemu ya kikosi cha Azam.

Wachezaji wapya waliotua kuziba nafasi zao wakashindwa kufanya hivyo na Fei Toto kujikuta akibeba mzigo mzito kuisaidia timu. Lakini ujio wa Florent Ibenge ukambadilisha akili. Akaanza kuona kwamba timu ina dhamira ya kweli ya kushindana ili kupata mafanikio.

Ibenge ni kocha mkubwa na mwenye mafanikio akiacha sifa njema kote alikopita. Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na AS Vita 2014. Fainali ya Kombe la Shirikisho akiwa na AS Vita 2018. Ubingwa wa Kombe la Shirikisho akiwa na Berkane 2022 na ubingwa wa CHAN 2016 akiwa na DRC ni mafanikio yanayomfanya kocha kuwa wa daraja la juu.

Uwepo wake Azam, ukaleta matumaini mapya kwa Fei Toto akiamini kwamba anachokitaka kwingine anaweza kukipata palepale Chamazi. Baada ya Ibenge kusaini akamtafuta Fei Toto na kumuahidi kujenga timu ya ushindani yeye akiwa sehemu muhimu ya timu hiyo. Yakaanza kushuka majina ya mafundi wa mpira. Sadio Kanoute, Jephte Kitambala na Pape Doudou Diallo yakatuma ujumbe chanya kwa Fei Toto. Hapo Fei Toto akaridhika kwamba sasa mpira utachezwa.

Akapiga simu yeye mwenyewe na kuomba mkataba asaini. Mabosi wake wakapagawa kwa furaha na akafuatwa kambini timu ya taifa na kusaini mkataba huo na kuwapa. Bila kupoteza muda tajiri Yusuf Bakhresa akaingia mtandaoni na kusema “He’s here to stay”…akimaanisha “Yupo hapa, anabaki”.

Siku chache baadaye majina matatu makubwa yakashuka. Hmid Baraket, winga hatari raia wa Tunisia akihudumu katika klabu ya CS Sfaxien, akasaini Azam. Issa Fofana, kipa mahiri wa Al Hilal ya Sudan mwenye uraia wa Ivory Coast, akatua Chamazi na Taeb Ben Zitoune, beki mahiri wa Al Hilal ya Sudan mwenye uraia wa Tunisia.

Hii ikakoleza mchuzi unaopikwa na Ibenge pale Chamazi na kuashiria mwaka wa mapinduzi kwa klabu hiyo. Feisal Salum msimu ujao atacheza chini ya kocha bora akizungukwa na wachezaji bora – yawezekana ukawa msimu bora zaidi kwake. Lakini yote hayo ni kutokana na wasifu wa Ibenge.

Katika hatua nyingine , Simba kupitia kwa msemaji wake Ahmed Ally walikana kumtaka Fei Toto, akihojiwa an vyombo vya habari hivi karibuni.

Ahmed amesema kuwa Sima hawajahi kutamani kutaka kumsajili Fei Toto wala kocha Fadlu hajawahi kutamka asajiliwe kwa msimu huu ujao wa ligi.

The post NYUMA YA PAZIA HUU…HIZI HAPA SABABU ZA FEI KUBAKI AZAM….SIMBA WAMKANA KWEUPEEE… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KISA CAF….. SIMBA vs YANGA MAPEMA TU MSIMU HUU….TFF WABADILI KANUNI CHAP….
Next Post KWA HILI LA SOWAH HUKO SIMBA….MMAMAAH….FADLU ATAJWA A-Z…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook