Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Utalii Wafunga Mwaka 2024/25 Ukiongoza Fedha za Kigeni

  • 47
Scroll Down To Discover

Ripoti mpya ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyotolewa jana Agosti 5, 2025 ikionesha takwimu za mwezi Juni, 2025, imethibitisha kuwa sekta ya utalii imefunga mwaka wa fedha ulioisha wa Serikali ikiongoza kwa kuleta fedha za kigeni nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo hadi Juni 30 mwaka huu, sekta hiyo imeendelea kuongoza kwa kuingiza Dola za Kimarekani Bilioni 3.934 ikiwa ni kutokana na ongezeko la watalii wa kimataifa la asilimia 10 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka mmoja wa fedha nyuma. Sekta ya madini imefuatia ikiwa na Dola Bilioni 3.67.

“Ni mwaka ambao filamu ya Royal Tour iliendelea kuonekana kupitia mitandao mikubwa duniani kama pbs ambako imeoneshwa katika televisheni zaidi ya 300 nchini Marekani lakini pia ni kipindi hiki pia mkakati wa filamu mpya ya Amazing Tanzania iliyomshirikisha Rais Samia na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi nayo iliingia sokoni kwa kuzinduliwa kule Beijing, China na kisha Novemba 2024 Dar es Salaam.

“Naweza kusema wazi mafanikio haya ni matokeo ya mikakati iliyohusisha viongozi wetu wakuu kabisa nchini kujitoa mstari wa mbele lakini usimamizi bora wa Wizara na mchango wa wadau ambao wamekwenda kote duniani nao kushiriki maonesho na kuitangaza nchi. Kama kuna jambo tutalisimamia mwaka huu ni kuja na mikakati zaidi. Tanzania inahitaji Dola na sisi ndio namba moja kuleta Dola. Tulale? Hapana. Ubunifu wetu hautakuwa na mwisho katika kuzileta Dola,” anasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, Dkt. Hassan Abbasi alipoulizwa msingi wa mafanikio hayo.



Prev Post Kesi ya CHADEMA Kusikilizwa Agosti 18, Mahakama Kutoa Uamuzi wa Zuio
Next Post HII HAPA TAREHE YA SIMBA, YANGA KUKUTANA MSIMU HUU…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook