
Mazishi ya kitaifa ya Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai, yanatarajiwa kufanyika Jumatatu Agosti 11i katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Alhamisi, Agosti 7,2025 na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, shughuli ya kuuaga mwili kitaifa itafanyika siku ya Jumapili kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Dkt. Tulia alitoa ratiba hiyo baada ya kufika nyumbani kwa marehemu eneo la Ndejengwa, jijini Dodoma, ambako pia alitoa pole kwa familia ya marehemu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!