
Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea na mpango wa kulifanya eneo linalotumika sasa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama SABASABA kuwa sehemu ya kivutio cha Utalii hata baada ya msimu wa maonesho hayo ili kuongeza wigo wa utalii wa ndani kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho hayo ya 49 yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Abbasi amesema kuwa, mafuriko ya watu wanaojitokeza kutembelea kwenye banda hilo ni matokeo chanya ya kazi kubwa iliyofanywa na Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza vivutio vya Utalii ndani na nje.
“Nimeona ongezeko la watu kila siku, kwa mfano nimeambiwa jana Jumamosi watu zaidi ya 40,000 wametembelea banda hili; hawa ni watalii muhimu sana tusiwaache.
“Tutazungumza na wenzetu wa Bodi ya Maonesho haya ili hili eneo miezi michache ijayo liwe endelevu kwa ajili ya utalii wa ndani liwe kama Bustani ya Wanyama yaani SABASABA ZOO,” alisema Dkt Abbasi.
Aidha Dkt. Abbasi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitoka na kutembea Banda la Maliasili na Utalii kujipatia huduma mbalimbali kutoka kwenye Idara na Taasisi zake na bustani ya wanyama ambapo maenesho hayo yataendelea mpaka Julai 13 mwaka huu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!