Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbeto Amvaa Zitto Akimtaka Aache Ubaguzi na Kudhalilisha Utu wa Watu

  • 41
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi kimelaani matamashi ya Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo ,Zitto Kabwe, aliyeshangazwa na kujitokeza Waandishi wa Habari, Watangazaji, Waigizaji na Wachekeshaji waliochukua fomu za kuwania Ubunge.

Vile vile , CCM kimemtaka Zitto ambaye ni Mbunge wa zamani wa Kigoma Mjini, kutambua hata wenye taaluma hizo, nao ni binadamu kama wengine.

Akizumgumza katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Kisiwani Unguja, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ameyaita matamshi hayo ya Zitto ni Ubaguzi wa wazi.

Mbeto alisema demokrasia ya Uchaguzi haibagui watu kwa rangi zao, Kabila, Dini au kwa kada zao Kitaaluma , badala yake kila mtu ana haki na Uhuru wa kuchagua au kuchaguliwa.

Alisema wakati Zitto akiwaponda Waandishi wa Habari, Watangazaji, Waigizaji na Wachekeshaji, Taifa la Ukraine hivi sasa, linaongozwa na Rais wake ambaye ni Mchekeshaji Volodymyr Zelensky.

Zelensky amezaliwa Januari 25 Mwaka 1978 ni Mwanasiasa, Mwandishi na Mwigizaji wa filamu, Mchekeshaji na sasa ndiye Rais wa Ukraine.

“Zitto ametoa matamshi ya dharau, kebehi na dhihaka iliopitiliza dhidi ya taaaluma hizo duniani kote . Alichokifanya ni unyanyasaji na udhalilishaji mbele ya macho ya dunia” Alisema Mbeto .

Aidha ,katibu huyo Mwenezi alisema CCM kina wanachama wenye taaluma na fani mbalimbali, hivyo hakitawazuia watu fulani ili kuwaruhusu kundi fulani, wachuke fomu na wengine wazuiwe.

“CCM ni taasisi kubwa ya kisiasa yenye wanachama toka makundi ya watu wenye uelewa, ufahamu,fani na taaluma kadha wa kadha. Istoshe si chama cha kibaguzi aidha kwa dini, rangi au asili za watu ” Alieleza

Katibu Mwenezi huyo alisema imekuwa ada na kawaida ya viongozi wa ACT Wazalendo , mara kadhaa kutumia lugha za kubagua watu kwa asili zao , nasaba na kabila ,huku wakikdhani hiyo ndio siasa safi.

“Hakuna makundi ya watu wenye alama na kusema hawa wanafaa kwa urais, ubunge ,udiwani au uwakilishi na wengine wasifae . Katiba ya nchi inataja usawa kwa binadami wote mbele ya katiba na sheria ” Alifafanua Mbeto

Mbeto alimtaka zitto kutoka na kusimama hadharani ili kuwaomba radhi waandishi wa habari ,waigizaji na wachekeshaji kutokana na matamshi yake yalioonyesha dharau ,Ubaguzi na udhalilishaji.



Prev Post Gonsalva Mlemavu Aliyehitimu VETA Anayepingana na Kazi ya Ombaomba
Next Post Cheza LOOT Legends Kutoka Meridianbet Uibuke Bingwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook