Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Gonsalva Mlemavu Aliyehitimu VETA Anayepingana na Kazi ya Ombaomba

  • 53
Scroll Down To Discover

Dar es Salaam 4 Julai 2025: Mwanadada Gonsalva Lungu kutoka Songea mkoani Ruvuma aliyezaliwa na mikono mifupi isiyo na viganja na mguu wa kulia mfupi ulioishia magotini mwa mguu wa kushoto amepingana kabisa na walemavu wanaoishi kwa kazi ya kuomba mitaani.

Akizungumza na Global Tv kwenye maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, Gonsalva amesema awali akiwa katika hali hiyo ilimkatisha tama na hakuona sababu ya kuishi kutokana na kunyanyapaliwa huku wengine wakimuogopa kwa kumuona kiumbe wa ajabu lakini maisha yake yalibadilika ghafla na kujiona ni miongoni kwa watu wenye thamani kubwa baada ya kujiunga na VETA.

Akiwa VETA Gonsalva alipata mafunzo ya ushonaji ambapo alifundishwa na walimu maalum kutokana na hali aliyokuwa nayo na kumfanya sasa hivi awe fundi mkubwa na kujiingizia kipato kinachomuwezesha kumtunza mama yake mzazi pamoja na ndugu zake wengine wasiokuwa na uwezo.

Miongoni mwa mavazi anayoshona na kudizaini kisasa kabisa mwanadada huyu ni pamoja na jezi za timu zenye muonekanao wa kisasa kabisa, nguo za watoto wakike na kiume pamoja na nyinginezo.

Gonsalva amewahi kuwashonea nguo baadhi ya viongozi na watu maarufu hali iliyomfanya asiisahau VETA na kuwaasa wenye uhitaji maalum wengine kuachana na dhana potofu ya uhitaji maalum wa kuombaomba na kwenda VETA ambapo wanaweza kuelekezwa ujuzi unaendana na hali walizonazo.

Alimaliza kusema mwanadada huyo huku akiishukuru VETA na kusema ndiyo mkombozi wake aliyemfuta machozi ya kutengwa, kunyanyapaliwa na kuonekana asingeweza kuwa msaada. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL   



Prev Post Rais Dkt. Samia Ashiriki Ufunguzi Wa Kanisa La Arise & Shine Kawe Dar -Live Video
Next Post Mbeto Amvaa Zitto Akimtaka Aache Ubaguzi na Kudhalilisha Utu wa Watu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook