

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu imetangaza hatua kali dhidi ya kijana anayefahamika kwa jina la “Cutting Master” kutokana na video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimwonyesha akiwauliza watoto maswali yenye maudhui ya kingono.
Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema tayari amewasiliana na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Kinondoni kuagiza timu ya wataalamu kufuatilia na kuchunguza kwa kina shughuli za kijana huyo, anayesemekana kuwa na ofisi katika eneo la Mwenge, Dar es Salaam.
“Nimepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kinyozi huyo, anayetuhumiwa kuwahusisha watoto katika maudhui yasiyofaa na kuyasambaza kwenye mitandao. Hili ni kosa kubwa linalokiuka Sheria ya Mtoto Sura ya 13 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao Sura ya 443,” amesema Dkt. Gwajima.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!