Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Said wa Tabata Mshindi wa Kwanza la Gari la SimBanking 2025

  • 35
Scroll Down To Discover

Mwaka umeanza vizuri kwa Said Mbaruku Mohamed, mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa gari wa kampeni ya Benki ni SimBanking Humu Tu, inayoendeshwa na Benki ya CRDB.

Mohamed anayefanya biashara ya nguo huko Tabata Magengeni, amejishindia gari jipya aina ya Toyota IST kutokana na kuwa kinara wa kutumia huduma za SimBanking kufanya miamala yake kila siku.

Akiendesha droo hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili kuna zawadi nyingi kwa wateja wanaotumia huduma za SimBanking zikiwemo fedha taslimu, kompyuta mpakato, magari aina ya Toyota IST, na kubwa zaidi, gari aina ya Toyota Harrier. Zawadi hizo zote amesema zinaendelea kutolewa hivyo akawataka wateja wa Benki ya CRDB kuendelea kuitumia SimBnaking kufanikisha miamala yao.

Hata wale ambao si wateja, Balozi wa kampeni hiyo, Frida Amani amesema ni wakati sasa wa kujiunga na Benki ya CRDB ili kuwa miongoni mwa wanaoweza kujipatia moja kati ya zawadi zilizopo.

Droo hiyo iliyochezeshwa mbele ya waandishi wa habari, ilisimamiwa na Lucy Katamba, mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

“Huu ni mwanzo tu, safari ya ushindi bado inaendelea!” amesema Adili.



Prev Post Nilidhani Bosi Wangu Ananichukia Kumbe Adui Yangu Halisi Alikuwa Rafiki Yangu wa Karibu
Next Post WAKATI FURAHA YA ‘KUIPOGOA’ SIMBA HAJAPOA….YANGA WASHUSHA MASHINE HII YA KAZI TZ….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook