

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma imetoa mahitaji katika kituo cha Watoto wenye uhitaji cha Safaad kilichopo katika kijiji cha Membe Chamwino Dodoma.
Baadhi ya mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na mafuta ya kupikia, Sabuni,Sukari, Unga wa Sembe, Mchele, Maharage, Nyama, Madaftari, dawa ya meno, miswaki, pipi, na kalamu.
Afisa Leseni Bw.Koyan Abubakar kutoka BRELA kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu alieleza kuwa Lengo kubwa ni kuwatia moyo Watoto na uongozi wa kituo hicho kwa kazi kubwa wanayoifanya ili kuongeza juhudi ya kuwahudumia wahitaji ili kufikia ndoto zao.
“BRELA ni taasisi inayosimamia usajili wa biashara na Leseni, imefika katika kituo hiki kwakua ni sehemu ya taasisi kushirikiana na jamii sio tu kutoa huduma za sajili, lakini pia kutoa huduma za kijamii” alisema Koyan.
Aidha Bw. Abubakar aliwaeleza Watoto wanaolelewa katika kituo hicho kuwa, wasifikiri kuwa ndoto zao zimezimika kwa kutokuwa na wazazi la hasha, kwakuwa wapo watu kama wao na hivi sasa ni viongozi wakubwa na hivyo wasikate tamaa, wasijisike wapweke kwakuwa wapo watu ambao wanajitoa kuwahudumia na kufafanua kwamba wapo Watoto wenye wazazi lakini wanapata changamoto.
“Njia kuu ya kufikia ndoto zenu ni kumuamini Mwenyezi Mungu, kuwa na makuzi mazuri kwa kufuata mafundisho mnayofunzwa na walezi wetu hapa kituoni, pili ili muweze kufikia ndoto hizo ni kufanya bidi katika masomo yenu shuleni, kuweni na maadili mazuri ili wanaowahudumia wasichoke ” alisema alisema Bw. Aboubakar.
Mkurugenzi wa kituo cha Watoto wenye Uhitaji na Waishio katika mazingira Hatarishi Safaad Membe Chamwino Bw. Adolph Alfred, ameishukuru BRELA na Serikali kwa ujumla kwa msaada huo ambao umetolewa kwao na kwamba ni kitu kikubwa sana, ambao utawawezesha Watoto hao kujikimu.
Bw.Alfred ameongeza kuwa, kituo hicho kilichopo Kijiji cha membe kinaleoa Watoto yatima ambao wametoka katika maeneo ya vijijini ndio mana aliamua kukiweka huko ili wakue katika mazingira yao, licha ya baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kwanini amekiweka kijijini ambako ni mbali na changamoto kufikika.
Kituo hicho kinalea Watoto 84 ambapo watoto 30 wanaishi hapo kituoni wakiwemo wasichana 18 na wavulana 12 wote ni wanafunzi ambapo walio shule ya msingi ni 17 na shule ya Sekondari ni wanafunzi 13 na Watoto 54 ambao wanahudumiwa wakitokea kwa walezi wao wanaokuja kupata mahitaji kituoni hapo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!