

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, atawania tena urais kwa muhula wa saba katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema Januari 2026, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa afisa mwandamizi wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).
Uchaguzi mkuu ujao utawahusisha wapiga kura kuchagua rais pamoja na wabunge. Museveni, mwenye umri wa miaka 80, Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya NRM, Tanga Odoi, Museveni anatarajiwa kuthibitisha rasmi nia yake ya kuwania tena siku ya Jumamosi.

“Rais atachukua fomu za kuonesha nia ya kugombea nafasi mbili; moja ni ya uenyekiti wa chama, na nyingine ni ya kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama ikiwa atapata nafasi hiyo,” alisema Odoi kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Katika uchaguzi wa mwaka 2026, mpinzani mkubwa anayeonekana kuwa tishio kwa Museveni ni Bobi Wine, mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa. Bobi Wine alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa mwaka 2021.Bobi Wine ameshathibitisha kuwa atawania tena urais mwaka ujao.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!