Bei ya mafuta duniani imepanda kwa kasi na kufikia kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha miezi mitano baada ya Marekani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya vituo muhimu vya nyuklia nchini Iran.
Bei ya mafuta ghafi ya Brent imepanda kwa asilimia 1.97 hadi kufikia Dola 78.53 kwa pipa, na mafuta ya West Texas Intermediate (WTI) yamepanda kwa asilimia 2.04 hadi kufikia Dola 75.35 kwa pipa.
Iran inatishia kufunga Mlango wa Hormuz, njia muhimu inayotumiwa kusafirisha mafuta kutoka Mashariki ya Kati, lakini wataalamu wanasema Iran ndiyo ina hatari kubwa ya kuathirika kuliko kunufaika.
Baada ya Marekani kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran, bunge la Iran liliidhinisha hatua ya kufunga mlango huo. Hata hivyo, uamuzi wa mwisho uko mikononi mwa Baraza la Usalama la Taifa la Iran.
The post Bei ya mafuta ghafi yapanda baada ya Marekani kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran appeared first on SwahiliTimes.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!