
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, akiambatana na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango, wameungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka kote duniani kushiriki Dominika ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohana wa Laterano lililopo Roma, Italia.
Ibada hiyo takatifu imeongozwa na Baba Mtakatifu – Papa Leo XIV, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kiimani ya Kanisa Katoliki Duniani.
Makamu wa Rais yupo nchini Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ubia wa Maendeleo kati ya Afrika na Serikali ya Italia (Mattei Plan) pamoja na mikutano mbalimbali ya uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Italia.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!