Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia: Wasichana Wasome Sayansi kwa Ajili ya Maendeleo ya Taifa – Video

  • 36
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa ujenzi wa shule maalum za wasichana kwa masomo ya sayansi unaoendelea kote nchini umelenga kutoa fursa kwa watoto wa kike kusoma masomo hayo, kwa kuwa taifa linawategemea katika maendeleo ya fani mbalimbali za kitaalamu.

Akizungumza leo, Jumatatu Juni 16, 2025, akiwa Bariadi mkoani Simiyu wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu, Rais Samia ametoa wito kwa jamii kuwaacha watoto wa kike na wa kiume wenye vipaji vya masomo ya sayansi kutumia fursa zilizopo ili kufikia malengo ya serikali ya kuwainua wanafunzi kielimu bila ubaguzi wa kijinsia.

“Shule hizi zimejengwa kwa huduma kamili; zina mabweni, nyumba za walimu karibu, mazingira salama na rafiki kwa kujifunza. Naombeni muwaachie watoto wa kike wenye akili nzuri wasome katika shule hizi. Majengo haya yamejengwa kwa ajili yao,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ametangaza kuwa serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu kwa Kanda ya Ziwa, inatarajia kujenga shule maalum ya masomo ya sayansi kwa wavulana mkoani Simiyu, hatua ambayo inalenga kuimarisha elimu ya sayansi kwa wanafunzi wote nchini.

Vilevile, Rais Samia amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea na ujenzi wa shule za ufundi na masomo ya amali katika kila mkoa wa Tanzania, ili kuwapa nafasi wanafunzi ambao hawatapata nafasi ya kujiunga na kidato cha tano au vyuo vikuu, kunufaika na elimu ya ufundi stadi.

STORI NA ELVAN STAMBULI, GPL



Prev Post Kesi ya Uhaini Yazidi Kupamba Moto, Lissu Asema Ananyimwa Haki Gerezani – Video
Next Post Mahakama Yaruhusu Lissu Kujitetea Kesi ya Uhaini – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook