

Dar es Salaam, 5 Mei 2025: Shirika la Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (DarTU), limeandaa mjadala wa kitaaluma uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam ambapo mwanahabari mkongwe Jenerali Twaha Ulimwengu ndiye aliyeongoza mjadala huo.
Mjadala ulikuwa na mada kuu ambazo ni: “Nafasi ya Wanataaluma katika Ujenzi wa Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025”, na umelenga kuibua hoja na fikra kutoka kwa wanataaluma, wahadhiri na wanafunzi kuhusu mchango wa taasisi za elimu ya juu katika kuhakikisha uchaguzi wa amani, mshikamano na demokrasia jumuishi nchini.

Global Peace Foundation (GPF) Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali ambalo, kwa zaidi ya miaka 15, limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya kuhamasisha amani na mshikamano katika jamii, likilenga makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo vijana, wanawake, viongozi wa dini, makundi ya watu wenye ulemavu, na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujenga jamii yenye maelewano, uwajibikaji na mafanikio ya pamoja.

Malengo ya Tukio:
- Kutoa jukwaa kwa wanataaluma na wanafunzi kujadili nafasi ya elimu ya juu katika kulinda na kudumisha amani kipindi cha uchaguzi.
- Kubaini mikakati na hatua za vitendo zinazoweza kuchukuliwa na vyuo vikuu katika kuhakikisha uchaguzi wa amani.
- Kukuza ari ya ushiriki wa wanataaluma na wanafunzi katika harakati za ujenzi wa amani ndani ya jamii.
- Kuelimisha juu ya umuhimu wa mijadala yenye ushahidi katika kukuza demokrasia na kuzuia migogoro ya kijamii.
-
Mhadhiri wa Chuo cha DarTU, Dkt. Lazaro Swai akizungumza kwenye mjadala huo.
Washiriki:
- Wahadhiri na wanataaluma kutoka vyuo vikuu mbalimbali vikiwemo DarTU, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Kampala, na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim.
- Wanafunzi wa elimu ya juu, hasa kutoka DarTU.
- Mzungumzaji mkuu alikuwa ni Ndugu, Jenerali Ulimwengu ambaye ni mtaalamu mwenye uzoefu mpana katika masuala ya amani, utawala bora na demokrasia.
-
Dkt. Denis kutoka Chuo cha Salim Ahmed Salim maarufu kama Chuo cha Diplomasia akichangia mada kwenye mjadala huo.
Matokeo Yanayotarajiwa:
- Kuongezeka kwa uelewa juu ya nafasi ya vyuo vikuu katika kujenga misingi ya amani kuelekea uchaguzi mkuu.
- Kuibuka kwa mikakati ya ushirikiano kati ya taasisi za elimu ya juu na mashirika ya ujenzi wa amani.
- Kukuza mtandao wa wanataaluma wenye dhamira ya kuendeleza amani na mshikamano nchini.
- Kuwezesha mijadala yenye msingi wa kitaalamu kuhusu demokrasia, haki za kiraia na uongozi jumuishi.
Tukio hili ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za GPF Tanzania katika kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika katika mazingira ya utulivu, haki, maelewano na mshikamano wa kitaifa.
Katika mjadala huo wanafunzi na wahadhiri walijadiliana mambo mbalimbali katika kuhakikisha uchaguzi Mkuu unajo unaotarajiwa kufanyika mwaka huu unakuwa wa salama na amani. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!