Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania Chaandaa Kongamano

  • 36
Scroll Down To Discover

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia Chuo cha Ukamanda na Unadhimu  Tanzania limeandaa Kongamano kuhusu  Usalama wa Kitaifa lililofanyika katika hoteli ya Gran Meria Jijini Arusha tarehe 6  Juni 2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman amekipongeza chuo hicho kwa kutengeneza jukwaa muhimu kwa wanataaluma ili kujadili maswala mtambuka hasa wakati huu ambapo kuna matishio mbalimbali yanayoikabili dunia.

Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania Meja Jenerali Justice Steven Mnkande

Aliwataka washiriki wa Kongamano hilo kujadiliana kwa kina mada zinazowasilishwa ili kuja na suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa kwa sasa na kwa siku zijazo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania Meja Jenerali Justice Steven Mnkande amesema kuwa kongamano hilo ni la kwanza kuandaliwa na chuo hicho likilenga mada tatu ambazo ni matumizi ya Akili Mnemba katika Ulinzi wa Taifa, Usalama wa Chakula kama Msingi wa Uimara wa Taifa na Usalama wa Nishati kwaajili ya Maendeleo Endelevu ya Taifa kwakuwa maeneo haya matatu yasipoangaliwa kwa kina yanaweza kuhatarisha Usalama wa Taifa.

Amesisitiza kuwa kongamano hilo litakuwa endelevu ili kutoa fursa  kujadiliana maswala mbalimbali yahusuyo Ulinzi na Usalama wa Taifa letu.

Aidha amesema kuwa makongamano yatakayoandaliwa baada ya hili yatakuwa ya kimataifa yakihusisha viongozi na wanataaluma kutoka nchi mbalimbali ili kubadilishana uzoefu katika kukabiliana na matishio hayo

Kongamano la kwanza la Usalama wa Kitaifa limewakutanisha Makamanda kutoka JWTZ, viongozi waandanizi wa serikali,wataalam bobezi katika nyanja mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na Wanafunzi wa kozi ya Ukamanda na Unadhimu kundi la 39 la mwaka 2024 hadi 2025.



Prev Post Balozi Nchimbi AONGOZA Waombolezaji Kumuaga Mzee Mongella
Next Post Majaliwa: Serikali Inatambua Mchango Wa Viongozi Wa Dini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook