HAWAJAWEKA wazi lakini tafsiri ya kiufundi ni kwamba Azam FC wako kwenye harakati za kujiandaa na lolote kwenye nafasi ya Feisal Salum ‘Fei Toto’
Staa huyo ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam amekuwa akihusishwa na kujiunga na Simba, Yanga na Kaizer Chiefs msimu ujao ambapo kila mmoja kwa wakati wake anapambana kupata ahueni ya dau. Azam wamekuwa wakisisitiza kwamba mchezaji wao anauzwa kwa zaidi ya Sh1 bilioni.
Ili kuziba pengo lake, Azam FC iko kwenye mazungumzo na Vipers ya Uganda kuhusu kiungo wake Allan Okelo ambaye Simba pia iliwahi kumtaka, lakini ilijibiwa kwamba mchezaji huyo hauzwi.
Hapo awali kikosi hicho kilipiga hesabu kubwa za kumsajili kiungo mshambuliaji, Okello ambaye naye ni fundi wa mguu wa kushoto kama ilivyo Elie Mpanzu.
SIMBA ILIFELI HAPA
Wekundu hao wa Msimbazi walimtaka Okello, kama kiungo mshambuliaji kupitia dirisha dogo la usajili lililofunguliwa Desemba 15 mwaka jana.
Utata kwa Simba kumpata Okello,ukawa kwa Rais wa klabu hiyo Lawrence Mulindwa, ambaye amekuwa mgumu kuachia mastaa wake muhimu wa kikosi hicho kuuzwa.
Taarifa za ndani kutoka Uganda zilisema kuwa: “Tumeanza mazungumzo na Azam wakimhitaji Okello, hatujamalizana lakini ni mazungumzo pekee ambayo hatujafikia mwisho.
“Unajua Okello anatakiwa na klabu nyingi, lakini hata sisi Vipers tunahesabu naye tutaona kipi tutafikia makubaliano kati yetu na Azam.”
Vipers inashika nafasi ya kwanza katika ligi ya Uganda ikiwa imecheza mechi 30, ikishinda 21,sare sita na kupoteza mitatu,huku Azam ikiwa namba tatu katika msimamo ikisalia na mechi mbili mkononi kati ya 30, huku Okello akiwa amefunga mabao 19 ndani ya msimu mmoja ambao huu ni wa pili tangu alipoanza kuitumikia Vipers katika mashindano hayo.
The post BAADA YA KUONA FEI TOTO ANAWEZA KUSEPA…AZAM WAHAMISHA NGUVU KWA STAA WA SIMBA.. appeared first on Soka La Bongo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!