Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NMB Yatangaza Gawio la Kihistoria na Matokeo Makubwa ya Fedha kwa Mwaka 2024

  • 8
Scroll Down To Discover

Gawio hili la kihistoria linaendana na dhamira ya Benki ya NMB ya ukuaji madhubuti wenye matokeo endelevu kwa wanahisa wake.

• Faida Kabla ya Kodi: Shilingi Bilioni 927, ukuaji wa asilimia 20 Mwaka hadi Mwaka

• Faida baada ya Kodi: Shilingi Bilioni 643 ukuaji wa asilimia 19 Mwaka hadi Mwaka

• Gawio kwa kila hisa: Shilingi 428.85 ukuaji wa asilimia 19 Mwaka hadi Mwaka

• Faida kwa kila hisa: Imefikia kiwango cha juu cha muda wote cha shilingi 1,287 Ukuaji wa asilimia 19 Mwaka hadi Mwaka.

Benki ya NMB imetangaza gawio la kihistoria kwa wanahisa la shilingi bilioni 214.43 na kufikia jumla ya gawio la Mwaka la shilingi Bilioni 214.43 kwa wanahisa wake kwa mwaka wa fedha ulioishia Desemba 31, 2024.

 Pendekezo na uamuzi huo ulipitishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa wanahisa na malipo ya gawio hili yanatarajiwa kufanyika tarehe 19 Juni 2025 au muda mfupi baada ya hapo, ukiwa ni Mwaka mwingine wa kuwahakikishia wanahisa thamani endelevu. Malipo ya gawio la shilingi bilioni 214.43 ni ongezeko la asilimia 19 ukilinganisha na malipo ya gawio lililolipwa Mwaka 2023 la shilingi bilioni 180.59

Mwaka 2024, Benki ya NMB iliendelea na mwendo mzuri wa utendaji ambapo Benki ilipata faida baada ya kodi ya shilingi bilioni 643 likiwa ni ongezeko la asilimia 19 ukilinganisha na mwaka uliopita. Utendaji mzuri wa benki uliimarisha nafasi yake ya kuendelea kuwa kiongozi na kama mmoja wa Benki zinazofanya vizuri zaidi Afrika Mashariki , na kiongozi wa kweli wa huduma za kifedha.

Mizania ya Benki iliendelea kuimarika,kutokana na kuwa imara kimtaji. Mikopo iliongezeka kwa asilimia 10 na kufikia shilingi trilioni 8.5 kutokana hasa na ukuaji wa ukopeshaji katika maeneo nyeti ikiwemo kilimo, sekta ya ujariamali, wateja binafsi, biashara kubwa na serikali.

Amana za wateja zilifikia Shilingi trilioni 9.6 likiwa ni ongezeko la asilimia 13 mwaka hadi mwaka kutokana na ukuaji wa amana katika maeneo yote nyeti ya biashara yetu. Kutokana na mwenendo mzuri wa mizania yetu, jumla ya mali za Benki ilikuwa kwa asilimia 13 mwaka hadi mwaka na kufikia shilingi trilioni 13.7. Benki iliendelea kuwa imara kimtaji ikiwa ndani ya ukomo wa kikanuni, na hivyo kuwa katika nafasi ya kuwa na biashara endelevu na nafasi ya uwekezaji wenye tija siku za usoni.

Moja ya kiashiria kikuu cha kikanuni kinaonesha maendeleo makubwa ya kiuwiano katika ufanisi na maboresho kwenye ubora wa mali na uwekezaji. Kufikia Desemba mwaka 2024, Benki ya NMB ilipata uwiano wa gharama na matumizi wa asilimia 38 ikilinganishwa na asilimia 39 ya mwaka 2023 hii ikiwa ni chini ya ukomo wa kikanuni wa asilimia 55, na kuifanya Benki ya NMB kuwa ni miongoni mwa Benki zenye ufanisi mkubwa nchini na katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.

Usimamizi wa hali ya juu wa ufadhiri na uwekezaji ikiwa ni pamoja na ubora wa vyanzo vya mikopo na usimamizi imara kulipelekea uwiano wa mikopo chechefu kushuka na kufikia asilimia 2.9 kutoka asilimia 3 ya mwaka uliotangulia. Uwiano huu wa Benki umeendelea kuwa ndani ya ukomo wa kikanuni wa asilimia 5 na chini ya wastani wa uwiano wa kisekta.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB Bwana David Nchimbi alisema “Malipo haya ya gawio yanatoa ishara thabiti ya maendeleo na ufanisi wa utekelezaji wa mkakati wetu, misingi imara ya utawala bora, na imani kubwa waliyonayo wanahisa wetu katika mipango yetu ya siku zijazo. Tunaendelea kujikita kwa ari katika kufungua fursa mpya za kimkakati za ukuaji wa huduma za kifedha,

kuboresha na kuimarisha huduma kwa wateja wetu, na kujenga ushirikiano wa kudumu wenye tija kwa pande zote. Lengo letu ni kufanikisha maono makubwa ya kuwa mshirika sahihi wa masuluhisho ya kifedha yanayotoa thamani kwa wateja, wawekezaji, na wadau wote kwa ujumla, kwa kuzingatia ufanisi, uvumbuzi, na uwajibikaji wa hali ya juu.”

Bwana Nchimbi aliongeza “Kwa Miaka ijayo, kupitia utekelezaji makini wa majukumu yetu ya utawala bora na uwajibikaji, Bodi ya wakurugenzi itaendelea kuwa kichocheo cha ukuaji wa muda mrefu wa benki na kutoa thamani endelevu kwa wanahisa wetu.”

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna alieleza yafuatayo “Mwaka 2024 ulikuwa ni mwaka wa kipekee kwa Benki ya NMB , ulioshuhudia maendeleo makubwa dhidi ya mkakati wetu, na kuongeza thamani kwa wadau wetu wote, ufanisi wa kiutendaji na malipo ya gawio hili kubwa kama ilivyopitishwa na wanahisa kunadhibitisha dhamira yetu ya kuwa na ukuaji madhubuti wenye matokeo endelevu.”

Shukrani zangu za dhati ziende kwa Serikali yetu, wasimamizi wa sekta ya fedha, wateja, wanahisa, na wafanyakazi wetu kwa mchango wao mkubwa na imani yao kwetu. Kutokana na ushirikiano huo, tumeweza kuanzisha na kuendeleza taasisi kubwa na endelevu, ikionyesha sifa ya kuwa kiongozi wa huduma bora kwa wateja, uvumbuzi wa kisasa, na utendaji wenye ufanisi wa hali ya juu.

Natoa shukrani za dhati kwa kuendelea kuwa sehemu ya safari hii, na tunatarajia kuendeleza mafanikio ya pamoja kwa kuimarisha ushirikiano wetu wa kipekee, kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu na thamani kubwa kwa wadau wote.
WhatsApp%20Image%202025-06-05%20at%2016.12.55
WhatsApp%20Image%202025-06-05%20at%2016.13.12
WhatsApp%20Image%202025-06-05%20at%2016.13.30%20(1)
WhatsApp%20Image%202025-06-05%20at%2016.13.30
WhatsApp%20Image%202025-06-05%20at%2016.13.43
WhatsApp%20Image%202025-06-05%20at%2016.16.02
WhatsApp%20Image%202025-06-05%20at%2016.16.33



Prev Post Makalla: Miaka Mitano ya Rais Samia Maendeleo Yameonekana Karatu
Next Post MAGAZETI ya Leo Ijumaa 06 June 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook