Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 05 June 2025

  • 22
Scroll Down To Discover

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 05 June 2025

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 05 June 2025

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 05 June 2025

Mwamuzi wa kati Hery Sasii, amefungiwa miezi sita na Bodi ya Ligi Kuu kwa kosa la kushindwa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati, kwenye mchezo kati ya Singida Black Stars na Simba uliofanyika Mei 28, 2025 hali iliyosababisha sintofahamu na malalamiko kutoka kwa timu husika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi leo Jumatano Juni 4, 2025, mwamuzi huyo alishindwa kutumia vizuri sheria za mchezo, jambo lililoathiri mwenendo wa mechi hiyo na kupelekea kutokuwepo kwa haki sawa kwa timu zote uwanjani.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.1) ya Ligi Kuu Tanzania inayohusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Kanuni hiyo inawataka waamuzi kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria za mchezo, bila upendeleo wala uzembe.

Kufungiwa kwa mwamuzi huyo kunakuja katika kipindi ambacho baadhi ya mechi za Ligi Kuu zimekuwa zikikumbwa na lawama kutoka kwa mashabiki na viongozi wa vilabu kuhusu utendaji wa waamuzi.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Fadlu Davids, amepigwa faini ya Sh2 milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa kosa la kutoa kauli zenye kuipotosha jamii kuhusu ratiba ya michezo ya klabu yake katika Ligi Kuu ya NBC.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Bodi ya Ligi, Fadlu alitoa matamshi hayo wakati akifanya mahojiano na Azam TV mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba na KMC uliofanyika Mei 28, 2025, katika Uwanja wa KMC Complex.

Katika mahojiano hayo, Fadlu alidai kuwa kuna ajenda tofauti zinazohusiana na upangaji wa ratiba ya michezo ya klabu yake, akionyesha kutoridhishwa na namna ratiba ya Ligi ilivyopangwa.



Prev Post Wasira Ateta Na Jaji Warioba, Mzee Butiku jijini Dar
Next Post DUH 🥺🥺…WAARABU TENA…..WAITIBULIA YANGA DILI LA MASHINE HII YA ‘KUMWAGA MAJI’….
Related Posts
© Image Copyrights Title

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 06 June 2025

© Image Copyrights Title

MAGAZETI ya Leo Jumatano 04 May 2025

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook