Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Aweka Jiwe La Msingi Jengo La ‘Viwango House’

  • 29
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 4 2025 ameweka jiwe la Msingi la ujenzi wa jengo la Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ‘Viwango Hause’ katika Hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi hiyo Njedengwa, Jijini Dodoma.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inatambua kuwa viwango vya ubora si tu vinahusiana na bidhaa bora, bali pia vinaimarisha afya na uchumi wa nchi.

Amesema kuwa viwanda vinapaswa kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kununulika hata nje ya nchi. “Tunataka mataifa mengine yakimbilie bidhaa zetu”

Ujenzi wa jengo hilo ambao umefikia asilimia 76 unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 25.3 ikijumuisha kodi ya ongezeko la thamani na gharama za mshauri elekezi

Jengo hilo linatarajiwa kukamilika Agosti 30, 2025.



Prev Post ALILIA KILA SIKU KWA KUNYIMWA MAPENZI, SASA AMEOLEWA NA MWANAMUME MWENYE UPENDO ANAYEMHESHIMU KILA SIKU
Next Post Makalla: The Royal Tour Imekuza Utalii Kaskazini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook