Dar es salaam, Meridianbet leo hii tarehe 31 Mei wamefika katika hospitali ya Palestina ambayo inapatikana Sinza ambapo kwaajili ya kutoa msaada wa vifaa vya afya kwa kinamama ambao wanajifungua.
Msaada huo umejumuisha vifaa mbalimbali vinavyotumika katika huduma za afya kwa akina mama wajawazito na wanaojifungua, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Meridianbet kuchangia kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto nchini.
Katika zoezi hilo lililofanyika leo, Meridianbet ilikabidhi pampers, mashuka safi, na sanitizers kwa akinamama wapya waliolazwa au waliokuwa wakihudumiwa hospitalini hapo. Lengo kuu la msaada huo ni kuwapa akina mama hao unafuu wa maisha baada ya kujifungua pamoja na kuhakikisha wanazingatia usafi na afya kwa mama na mtoto.
Akizungumza wakati wa tukio hilo,Mhariri wa Meridianbet Nancy Ingram alisema kuwa, “Tunaamini kuwa afya ya mama ni msingi wa jamii imara. Kupitia msaada huu, tunalenga kuunga mkono juhudi za serikali na taasisi za afya katika kuhakikisha kila mama anapata huduma bora na salama wakati wa ujauzito na kujifungua.”
Mzigo mkubwa unapatikana ndani ya Meridianbet leo hii mechi ya fainali ya Uefa. Suka jamvi lako hapa lakini pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.
Kwa upande wa hospitali hiyo baada ya kupokea msaada wa vifaa hivyo kutoka kwa Meridianbet walisema kuwa, “Msaada huu umetufariji sana. Vifaa hivi ni muhimu sana, hasa kwa wale wakina mama wanaokosa baadhi ya mahitaji baada ya kujifungua. Tunawashukuru Meridianbet kwa moyo wa upendo na kujitolea.”
Meridianbet imeendelea kuwekeza kwenye miradi ya kijamii katika sekta ya afya, elimu, michezo, na maendeleo ya vijana. Tukio hili ni mwendelezo wa jitihada hizo za kuleta mabadiliko chanya kwa Watanzania.
Lakini vilevile kama inavyojulikana kuwa kampuni hii kubwa ya ubashiri inajihusisha na michezo ya bahati nasibu, leo hii kuna fainali ya Ligi ya mabingwa ulaya kati ya PSG vs Inter Milan hivyo ingia kwenye akaunti yako uweze kubashiri mtanange huu.
Meridianbet wao wamempa nafasi kubwa ya kushinda mwenyeji kwa ODDS 2.27 kwa 3.50. Je wewe leo hii unampa nani kuondoka na ushindi?
The post MERIDIANBET YATOA VIFAA VYA AFYA HOSPITALI YA SINZA…. appeared first on Soka La Bongo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!