
Sikuwahi kufikiria siku moja ningefutwa kazi bila hata kupewa sababu. Ilikuwa siku ya Ijumaa asubuhi nilipoitwa ghafla ofisini kwa meneja. Nilipofika, nilikabidhiwa barua na kuambiwa huduma zangu hazihitajiki tena. Nilihisi dunia inazunguka, moyo ukasita kupiga kwa sekunde kadhaa. Nilishindwa hata kuuliza kwa nini. Niliondoka ofisini nikiwa na machozi yakinitiririka, nikihisi aibu na huzuni kubwa.
Wiki ya kwanza nyumbani ilikuwa mbaya zaidi. Niliamka kila asubuhi nikijiuliza kosa langu lilikuwa lipi. Niliogopa kukutana na majirani au marafiki kwani sikutaka kuulizwa maswali. Kila usiku nililala nikiwa na mawazo mazito, nikijiuliza maisha yangu yangeendeleaje bila kipato. Nilikuwa nimezoea maisha yenye ratiba na mshahara wa kila mwezi. Mara ghafla nikawa sina kazi, sina mpango, na sina uhakika wa kesho.SOMA ZAIDI
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!