Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

WAKATI SIMBA WAKIIPIGA JICHO TAREHE 16…..MPANGOWA YANGA HUU HAPA….

  • 5
Scroll Down To Discover

KLABU ya Yanga imeanza mikakati kabambe ya kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, unaotarajiwa kupigwa, Septemba 16, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais, Arafat Haji, amesema juzi kuwa mipango na mikakati ya mechi hiyo imeshaanza ambapo lengo ni kupata ushindi ili kuendelea kulihifadhi taji hilo.

Alisema kuwa heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26, itaanza kuwekwa katika mchezo huo.

“Tuna kazi tarehe 16, jamaa walitamani ule mfumo ungeendelea, walitamani ungendelea kuchezwa kwa mfumo wa nusu fainali ili watukimbie tena, lakini wanasema Mungu si Athumani, kawaleta, siku hiyo tutaanza kuweka heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26,” alisema Haji.

Akaongeza: “Tutakwenda kuhakikisha Ngao ya Jamii inakwenda nyumbani, ibakie Jangwani kwa sababu ni kwao, hivyo ushirikiano wa Wanayanga wote ule uliooneshwa msimu uliopita uongezeke mara dufu msimu huu.”

Hivi karibuni, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lilitangaza mabadiliko ya Kanuni ya Ligi Kuu msimu huu ambapo badala ya kucheza mechi tatu, nusu fainali mbili na fainali moja, kwa timu nne kushiriki, badala yake itacheza mechi moja tu.

Kwa mujibu wa TFF, mchezo huo utahusu bingwa wa Tanzania Bara ambaye ni Yanga, watakaocheza na mshindi wa pili wa Ligi Kuu, Simba.

Imesema timu hizo zitalazimika kucheza mechi hiyo kutokana na kanuni. Yanga ilibidi icheze na bingwa wa Kombe la FA, lakini kwa sababu yenyewe ndiye bingwa pia wa makombe yote mawili, hivyo kanuni inasema itacheza na mshindi wa pili wa Ligi Kuu.

TFF, ilifafanua kuwa mfumo wa mashindano hayo umebadilika msimu huu kutokana na marekebisho ya kanuni zilizopitishwa hivi karubuni na Kamati ya Utendaji ya TFF.

Moja ya marekebisho hayo yanasema ikitokea mazingira kama ya sasa ambapo mashindano yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) yamebana ratiba za TFF itachezwa mechi moja tu ya Ngao ya Jamii.

Kwa sasa Tanzania ni mwenyeji wa fainali za CHAN zilizoanza Agosti 2 mwaka huu, zitakazomalizika Agosti 30.

Kwa mfumo wa kawaida, Yanga ilitakiwa kucheza dhidi ya Azam FC, katika mchezo wa nusu fainali, huku Simba ikitakiwa kucheza dhidi ya Singida Black Stars.

Yanga imeifunga Simba mara tano mfululizo, mara nne kwenye mechi za Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo, nyumbani na ugenini pamoja na mchezo mmoja wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii uliochezwa, Agosti 8, mwaka jana.

Msimu uliopita, Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii kwa kuichakaza Azam, mabao 4-1 yaliyofungwa na Prince Dube, Yoro Diaby aliyejifunga mwenyewe, Stephane Aziz Ki na Clement Mzize, huku bao la Azam ambao walitangulia likifungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ Agosti 11, mwaka jana, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

The post WAKATI SIMBA WAKIIPIGA JICHO TAREHE 16…..MPANGOWA YANGA HUU HAPA…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BAADA ATEBA KUUZWA SIMBA…EDO KUMWEMBE ATUPA DONGO KWA FADLU….
Next Post KUELEKEA MSIMU MPYA ….FADLU AITILIA NGUMU CAF MAPEMAAH….AFUNGUKA ISHU YA ZNZ……
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook