Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

ACT Wazalendo Wafanya Kikao Maalum cha Kamati Kuu Kuhusu Uteuzi wa Mwisho wa Wagombea

  • 3
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Ndugu Othman Masoud, leo Agosti 21, 2025, anaongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu kinachoendelea hivi sasa katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema, Jengo la Maalim Seif, Magomeni – Dar es Salaam.

Kikao hicho kimeitishwa mahsusi kwa ajili ya kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa ubunge na uwakilishi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kwa mujibu wa viongozi wa chama hicho, kikao hiki kinachukuliwa kuwa ni hatua muhimu ya mwisho kabla ya wagombea hao kuridhishwa rasmi na kupokea baraka za chama kwa ajili ya kupeperusha bendera za ACT Wazalendo katika maeneo mbalimbali nchini.

 



Prev Post NAFASI Za Kazi Reuna Group
Next Post Vodacom Tanzania Yaripoti Ukuaji Imara Uliochagizwa Na Azma Yake Ya Kugusa Jamii Kwa Mwaka Wa Fedha 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook