Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Watano kati ya 19 waliokuwa wabunge Chadema wateuliwa CCM

  • 3
Scroll Down To Discover

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) imewateua miongoni mwa waliokuwa wabunge 19 wa Chadema kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Wabunge hao walihamia CCM baada ya kuvunjwa kwa Bunge la 12, na sasa wamepata nafasi ya kugombea kupitia chama hicho tawala.

Akizungumza leo Jumamosi, Agosti 23, 2025, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, ametangaza rasmi majina ya waliopitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika majimbo mbalimbali.

Miongoni mwa walioteuliwa ni:

  • Esther Matiko – Tarime Mjini

  • Ester Bulaya – Bunda Mjini

  • Hawa Mwaifunga – Tabora Mjini

  • Kunti Majala – Chemba

  • Jesca Kishoa – Iramba Mashariki

Makalla amesema uteuzi huo ni sehemu ya dhamira ya chama kuendeleza demokrasia ya ushindani huku kikitoa nafasi kwa viongozi wenye uzoefu na uwezo wa kisiasa kuwatumikia wananchi.

Uamuzi huo unakuja baada ya kikao cha NEC kilichofanyika Agosti 23, 2025 kupitisha majina ya wagombea wa majimbo yote ya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na wawakilishi wa viti maalum.



Prev Post Hii hapa orodha kamili waliopenya ubunge, uwakilishi CCM
Next Post Dk. Asha-Rose Migiro Ateuliwa Katibu Mkuu Mpya wa CCM
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook